karibuni

chuki ikiingia ndani kupitia mlangoni upendo hutoka nje kupitia dirishani,upendo unagharama sana ukilinganisha na chuki,afadhali kununua upendo kuliko kuzawadiwa chuki na migogogro

March 05, 2007

accoustic design and analysis

Wakati wa kubadilisha mtazamo wa kibaguzi umeanza kuingia polepole hapa ujerumani kwani kwa wiki mbili nimekuwa katika kongamano la kuondoa urangi na udini kwa wageni waishio hapa.Hili limefanyika katika mradi wa kudumisha muingiliano wa tamaduni kati ya nchi za ulaya na zile zisizo za ulaya.jina la mradi huu ni Sepela lenye maana ya furahi ambapo mlengo wake ulizamia zaid kuanzia shule za chekechea hadi shule za msingi ambapo tunatarajia kufanya makongamano na wanafunzi wasiopungua 4000 kwa kipindi cha miaka miwili huku tukibadilishana tamaduni na mila zetu na kujenga daraja la maelewano kati yetu.mpango huu unadhaminiwa na halmashauri ya jiji la München ambapo wajumbe wote wameonyesha mvuto mkubwa katika hilo.nitakuwa nikiwaletea yaliyojiri katika maendeleo ya mpango huu.Nina imani kuwa watoto watakuwa ni njia rahisi ya kutumbukiza mtazamo huu kwani wale waliokwisha kuwa na umri mkubwa tayari wamesha ivaa kasumba hii ya ubaguzi.

1 comment:

Egidio Ndabagoye said...

Ulipotea kaka.Tunasubiri michapo kibao nyingi toka hapo.