karibuni

chuki ikiingia ndani kupitia mlangoni upendo hutoka nje kupitia dirishani,upendo unagharama sana ukilinganisha na chuki,afadhali kununua upendo kuliko kuzawadiwa chuki na migogogro

September 15, 2010

September 01, 2010

MAMBO KAMA KAWAIDA


You must be informed of what is nice for you,mhhhhhhhhh day to day comes something nice for you.check out this!!!! another utamu ndani ya München if you want to be left behind then miss this,many things happen but few are nice for you so come one and all and see by yourself.oohhhh don´t forget I will be there so cheers.lastly with your partner will be even more sweet.see you there guys

August 20, 2010

PARTY PARTY ONCE AGAIN

Once again after so much boring moments,Africans in München are cordially invited for a party which lasts for two days,just read the flier above and know by yourself friday Party and saturday Party.the place is just 6minutes from haupt bnf U1 richtung mangfall plz and the rest is on the flier,All African music is of concerned so come and hear your favorite.

July 23, 2010

nimerudi tena

kuna mambo mawili makubwa ninahitaji kuyasema leo,la kwanza ni kufukuzwa kwa waafrika kutoka nchi ya naijeria huko Afrika ya kusini,nimepata habari jana kuwa kuna wanaijeria 47 ambao kwa kweli kuwapatia dakika tano ili wawe katika uwanja wa ndege na wakati wamekuwa wakiishi kihalali tena kwa kulipa kodi?????mbali na hapo kuna dada mwingine mdogo wa mri wa miaka isiyozidi 24 hapa ujerumani, amepewa siku nne tu kurudi nyumbani Kenya wakati hata pesa ya kupata mkate wa chai asubuhi kwa siku 120 alizoishi hapa hakuwa amelipwa.mhhhhhh inakuwa ngumu sana kwangu kuelewa hilo,au ina maana na sisi waafrika tuanze kuwafukuza wendawazimu hawa ambao wametufanya tuwe watumwa kwao????????naishia hapo kwa kuwa nitakasirika bure.hii si khaki

July 04, 2009

PAPY NGUZA

nawasalimu watu wote kwa jina la aliye juu,leo siongei mengi ila ninauliza kama kuna kati yetuanayejua ukweli kuhusiana na kesi ya mkongwe Nguza Viking na wanae jela,nina mtazamo tofauti na ukumu ya kifungo cha maisha dhidi yao kwa kuwa ninashindwa kuamini mashtaka yao yana ukweli wa kiwango kipi.baba na wanae kutenda kosa la namna hiyo kwangu inaniwia vigumu kuamini,au kuna mkono wa mtu au sababu nyingine tofauti na hiyo?nashindwa kufahammu ni namna gani mkono washeria unavyotenda wajibu wake ingawa unaheshimika.ninatoa mwito kwa wanaohusika kuangalia tena kesi hii kwa kuwa nadhani kuna zaidi ya hapo.Ninawatakia kheri wana blog wote na wapenda khaki na amani

May 23, 2009

UMEME JAMANI

bado ninasikitika kuona kuwa hadi sasa swala la umeme ni tatizo sugu Tanzania na nchi zilizo jirani, yaani tunategemea hadi lini tutakuwa na matatizo ya umeme ambao umetafuna fedha za walipa kodi kwa muda mrefu hivi.viongozi wa nchi hizi wanafikiria nini kuhusu wazalendo wanaoishi kwa chini ya dola moja ya kimarekani kwa siku na hapo hapo kulipa kodi ambayo yote inaishia kwa wakubwa na bado umeme ni tatizo sugu vile vile!!!!!!!!naomba tuogope kula tusichopanda kwa sababu si haki yetu tuwape wananchi UMEME nao wawe na amani.umeme unakatika hata katika kiwanja cha ndege hii ni aibu gani jamani?

December 13, 2008


FISADI ANYAKULIWA MAREKANI:
Haya,ninapenda kutoa wito kwa viongozi wa nchi za Africa kufuata mfano wa uadilifu kama tulivyoona pale Marekani wakati gavanaRod Blagojevich wa jimbo la illinois alipotiwa mbaroni kwa tuhuma za rushwa na ufisadi.gavana huyu anatuhumiwa kujaribu kuuza kiti cha seneta Obama alichokiacha wazi baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani mapema November mwakaa huu.cha msingi hapa ni kuangalia jinsi swala zima la rushwa linavyo fuatiliwa kwa haraka,ukilinganisha na nchi za Afrika ambapo ushaidi wa wala rushwa upo lakini inachukua miaka hata sita kwa watuhumiwa kutiwa katika mkono wa haki au hata wasishtakiwe kabisa.