FISADI ANYAKULIWA MAREKANI:
Haya,ninapenda kutoa wito kwa viongozi wa nchi za Africa kufuata mfano wa uadilifu kama tulivyoona pale Marekani wakati gavanaRod Blagojevich wa jimbo la illinois alipotiwa mbaroni kwa tuhuma za rushwa na ufisadi.gavana huyu anatuhumiwa kujaribu kuuza kiti cha seneta Obama alichokiacha wazi baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani mapema November mwakaa huu.cha msingi hapa ni kuangalia jinsi swala zima la rushwa linavyo fuatiliwa kwa haraka,ukilinganisha na nchi za Afrika ambapo ushaidi wa wala rushwa upo lakini inachukua miaka hata sita kwa watuhumiwa kutiwa katika mkono wa haki au hata wasishtakiwe kabisa.
No comments:
Post a Comment