karibuni

chuki ikiingia ndani kupitia mlangoni upendo hutoka nje kupitia dirishani,upendo unagharama sana ukilinganisha na chuki,afadhali kununua upendo kuliko kuzawadiwa chuki na migogogro

May 23, 2009

UMEME JAMANI

bado ninasikitika kuona kuwa hadi sasa swala la umeme ni tatizo sugu Tanzania na nchi zilizo jirani, yaani tunategemea hadi lini tutakuwa na matatizo ya umeme ambao umetafuna fedha za walipa kodi kwa muda mrefu hivi.viongozi wa nchi hizi wanafikiria nini kuhusu wazalendo wanaoishi kwa chini ya dola moja ya kimarekani kwa siku na hapo hapo kulipa kodi ambayo yote inaishia kwa wakubwa na bado umeme ni tatizo sugu vile vile!!!!!!!!naomba tuogope kula tusichopanda kwa sababu si haki yetu tuwape wananchi UMEME nao wawe na amani.umeme unakatika hata katika kiwanja cha ndege hii ni aibu gani jamani?