karibuni

chuki ikiingia ndani kupitia mlangoni upendo hutoka nje kupitia dirishani,upendo unagharama sana ukilinganisha na chuki,afadhali kununua upendo kuliko kuzawadiwa chuki na migogogro

July 04, 2009

PAPY NGUZA

nawasalimu watu wote kwa jina la aliye juu,leo siongei mengi ila ninauliza kama kuna kati yetuanayejua ukweli kuhusiana na kesi ya mkongwe Nguza Viking na wanae jela,nina mtazamo tofauti na ukumu ya kifungo cha maisha dhidi yao kwa kuwa ninashindwa kuamini mashtaka yao yana ukweli wa kiwango kipi.baba na wanae kutenda kosa la namna hiyo kwangu inaniwia vigumu kuamini,au kuna mkono wa mtu au sababu nyingine tofauti na hiyo?nashindwa kufahammu ni namna gani mkono washeria unavyotenda wajibu wake ingawa unaheshimika.ninatoa mwito kwa wanaohusika kuangalia tena kesi hii kwa kuwa nadhani kuna zaidi ya hapo.Ninawatakia kheri wana blog wote na wapenda khaki na amani

1 comment:

ARUSHA SEKII ALUMNI said...

hope imekuwa muda mrefu sana kabla sijajibu swali lako lakini sasa ninakuhakikishia nitajibu ingawa nina huzuni kubwa kwa haki na amani kwa nchi za afrika,nimerudi tena