karibuni

chuki ikiingia ndani kupitia mlangoni upendo hutoka nje kupitia dirishani,upendo unagharama sana ukilinganisha na chuki,afadhali kununua upendo kuliko kuzawadiwa chuki na migogogro

March 24, 2007

JAMANI TUNAFIKIRA GANI JUU YA MTU HUYU?
Ndugu Munishi (mchungaji kama unavyojiita)ninakubaliana na mada zako nilizozisoma kwa makini sana, kwa bahati mbaya sana ninasikitika kukufahamisha kuwa siafikiani hata kidogo na mtazamo wako wa kisiasa kwa kuwa kwa upande wangu naona kama unaweweseka sana kimawazo na wala usipoteze muda wako kufikiria kuna siku utakuwa Rais Mteule wa Tanzania,kuna maovu mengi ya serikali ambayo umeyaongea lakini inaonekana wewe utafanya mbaya zaidi.umezungumzia kuinua kiwango cha elimu Tanzania iwapo utachaguliwa kitu ambacho ungeweza na unaweza kukifanya hata kama wewe si Rais(kuna watu wengi wamejenga mashule na kusomesha yatima wakati hawana hata cheo cha balozi wa nyumga kumi).ukanigusa zaidi kuhusu udini ukimkashifu Rais kwa kushiriki katika kuchangisha fedha za kujenga makanisa kwa kuwa tu yeye ana imani tofauti na yako,umeongea pia kuwa endapo utakuwa rais utaanzisha serikali ya injili yenye katiba ya injili na mleongo wa injili,mmmmmm kumbuka wewe ni mchungaji kama unavyojiita na kiongozi mwenye ubaguzi wa namna yeyote kwa watu anaotaka kuwaongoza hastahiki kabisa kuwa kiongozi,Yesu Krisoto alisema "nimekuja duniani ili ulimwengu uokolewe"sasa wewe unayeanza kuingiza udini katika kuutamani utamu wa ikulu mimi naona utakuwa hatari kuliko nyoka anayeitwa KOBOKO.Kumbuka si wewe pekee unayefahamu maovu ya watawala waliopita si tu katika Tanzania bali duniani kwa ujumla wengi tunafahamu hivyo kwa hiyo tumia busara kutafuta urais na mimi ninakutakia kila la kheri ingawa kura yangu huipati kabisa.wakati unajibu hoja ya lugha ya kiingereza umekosea mahali fulani kusema kuwa rais mstaafu bwana mkapa ana uwezo finyu wa lugha hiyo,ninaomba nikushauri kuwa siku zote kama huna ufahamu wa kitu kwa mapana basi utaona watu wengine pia kuwa ni maimuna kumba hiyo ni tafsiri tofauti na ukweli,nakushauri kufanya utafiti wa kina kabla ya kuongea hasa kuandika mada kwani ni vema kuandika mada yako kwa usahihi kuliko kutumia jazba kufanya hivyo wakati unataka kuwa rais.Mwisho ningekushauri uendelee na uimbaji kwa kuwa ninakumbuka nyimbo zako nyingi nzuri kuliko mada unazoziandika sasa.Wimbo wako ninaoupenda sana ni kinko mbali ugenini, endelea na kipaji chako cha uimbaji na ninakutakia mafanikio mema na safari yako ya IKULU

2 comments:

chomola said...

Mbona mnamsakama Munishi? Kosa lake ni kusema kwamba anataka kuwa rais? Au kusema CCM imezeeka? Watanzania msipoamka mtalaliwa na CCM mpaka mwisho wa dunia. Kwangu mimi naona Munishi hajakosea kutoa maoni yake. Hata kama maoni hayo yatatofautiana na yale ya wanachama wa CCM hiyo ilitegemewa.Lakini kujaribu kumnyamazisha Munishi ili CCM iendelee kuwaua watanzania huo ndio upumbavu ambao Munishi amekuwa akiukemea kwenye maelezo yake.Kwamba ameweza kujieleza mpaka serikali ya Mkapa ikaamua kuipiga marufuku kanda yake, hiyo inaonyesha jinsi Munishi alivyo tishio kwenu mnaojiita wasomi kumbe ni geresha tu. Iweje wasomi wapoteze muda kujibizana na huyo mnayemwita mjinga Munishi?Mimi siyo muumini wa Munishi, lakini naheshimu uhuru wake wa kutoa maoni. Na mengi ya maoni yake ni kweli na yana msingi kabisa. Siyo busara kuyapuuza maoni eti kwa sababu alieyatoa ni Munishi. Mnaotaka kuikumbatia CCM endeleeni kufanya hivyo kwa hasara yenu. Na kama Munishi ameamua kuipinga CCM hiyo ni haki yake kikatiba kwani Tanzania ni nchi ya vyama vingi. Pale Munishi anaponiacha hoi, ni wakati anaposema yeye siyo mwanachama wa chama chochote cha kisiasa, lakini anataka kuwa Rais wa Tanzania.Hapo tu ndipo ambapo simuelewi, lakini hiyo hainipi haki ya kuyapuuza maoni yake. Pengine anajua jinsi atakavyoyatimiza malengo yake bila chama cha kisiasa. Tumpe muda na tumsikilize pengine yeye ndiye mkombozi wa Tanzania