karibuni

chuki ikiingia ndani kupitia mlangoni upendo hutoka nje kupitia dirishani,upendo unagharama sana ukilinganisha na chuki,afadhali kununua upendo kuliko kuzawadiwa chuki na migogogro

September 28, 2007

KWAHERI MZEE KADUMA


Ni habari ya masikitiko niliyoipata leo saa nne asubuhi toka kwa mchumba wangu msanii Hawa Chekanae kuwa Mzee godwin Kaduma ametutoka.nilipatwa na mshituko lakini nimekubali matokeo kwani sina budi.ninamkumbuka sana mzee kaduma hasa kwa utani na ucheshi wake hasa wakati nilipokuwa nikisoma chuo cha sana na wakati wa jioni tulipokuwa tukitwanga KONYAGI katika baa iliyojulikana kama TOP LIFE.kuna mengi ya kusimulia kutokana na marehemu Kaduma hasa kwa ufuatiliaji wa maadili ya utamaduni na sanaa ya kiafrika.ninakumbuka niliwahi kumtania Mzee Kaduma kuhusu gari lake kuu kuu alilolipenda sana aina ya peugeout,nakumbuka nikimwambia"mzee kaduma kesho unakwenda Dar? nilipenda kuomba lift lakini ninaogopa kuchelewa kwa kuwa gari lako ni chovu sana"naye alinijibu "nenda kanunue la kwako jipya kisha utanikuta dar"Mungu akulaze pema peponi.

6 comments:

luihamu said...

Karibu sana Ras,nimefurahi ujio wako,tuendeleze libeneke la U-RASTA NA TOBOMOE BABYLOAN WALLS.


Mzee Kaduma,Jah live.

Egidio Ndabagoye said...

Ras pole sana kwa kuondokewa na mama mzazi.tupo pamoja kaka wakati wote.
karibu tena

kingo said...

nashukuru sana ndugu zangu,nimerudi salama na ninaendelea na libeneke la kuutetea uafrika.asante sana Egidio kwa pole yako ni kweli ni ngumu kusahau msiba huu wa mpendwa mama yangu lakini imebidi nikubali matokeo japo kwa uchungu mwingi,Luihamu nashukuru pia nimerudi kamanda

Simon Kitururu said...

Samahani, natoka nje ya somo!

Njoo tumalizie kujadili kipengele, ili tuende kwenye hatua nyingine ya kuboresha wanajumuiya wa jumuiya ya Watanzania wanao tembelea au wanao blogi.

Tembelea hapa : http://blogutanzania.blogspot.com/
ilia tumalize kujazia dondoo ili tu anze na kipengele kingine.
Idumu JUMUWATA!

Simon Kitururu said...

Ras Pole sana Mkuu!
Tuko Pamoja!

kingo said...

asante Kitururu kwa kutukumbusha mjadala ambao utatufanya tuendelee mbele badala ya kubaki nyuma.Ninaingia sasa hivi kwenye kishiriki mjadala huo.nakutakia kazi njema na siku njema.
Ras