karibuni

chuki ikiingia ndani kupitia mlangoni upendo hutoka nje kupitia dirishani,upendo unagharama sana ukilinganisha na chuki,afadhali kununua upendo kuliko kuzawadiwa chuki na migogogro

October 12, 2007

WANA MAZINGIRA WAHAMASISHA MUNICH


Mradi wa utunzaji wa mazingira leo umeandaa kampeni ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa kuweka mkutano wa hadhara wakieleza umuhimu wa mazingira,mkutano huo umefanyika leo katika mtaa mkubwa wa kibiashara na shughuli za kitalii ujulikanao kama KARLSPLATZSTAKHUS hapa munchen.nilibahatika kupita hapo na kusikiliza yaliyozungumzwa ikiwa ni pamoja na kuiomba serikali kuongeza fungu la kusaidia utunzaji wa mazingira na kuhimiza mafunzo ya awali katika shule juu ya elimu ya mazingira na umuhimu wake.nilijiuliza swali dogo,je uhamasishaji huu unatilia mkazo hasa mazingira ya nchi hizi tu? wakati kuna mlimbikizo wa viwanda na shughuli nyingine zinazoharibu mazingira katika nchi za afrika bla kujali madhara yake katika nchi hizo?na je ni kosa la nani kati ya wawekezaji hao na serikali za nchi husika?jibu tunalo wenyewe kazi kwetu sasa.

2 comments:

luihamu said...

Ras mzima,safi sana.
tuko pamoja.

kingo said...

mimi mzima kaka sijui wewe.amani na upendo dread.