MJUE TENA KIANGI LUFULONDAMA
Kuna mtu watu wengi hawajawahi kumsikia, jina lake ni hilo hapo juu,bwana huyu amezalia katika mkoa wa Mwanza wilaya ya magu tarehe 04/07/1974 alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Mkula kuanzia mwaka 1982 hadi mwaka 1988 na kisha akakanyaga elimu ya saekondari kwa jina ni Takwa sec huko huko kwenye kashfa ya muheshimiwa Mbilinyi mwaka 1990 hadi mwaka 1993 na hatimaye akakamata uhamisho wa elimu ambao watu wengi hutafuta na kukosa na kisha kujikuta amekanyaga Moshi sec ambayo watu wengi huiita Moshi sekondari skuul kati ya mwaka 1998 hadi mwaka 2000, huyu mtu alitafuta elimu peke yake nilisahau kuwaambia.mwaka huo huo alijaribu kutafuata maisha na kujikuta ameangukia mbinga mkoa wa Ruvuma ambako alikuwa mratibu msaidizi wa mpango wa kuelimisha walimu wa shule za msingi ambao hawakupata nafasi ya kupata elimu aliyoipata.alifanya kazi kwa mwaka mzima uliokuwa umetingwa na matatizo mengi ambayo kila mmoja wetu anaweza kufahamu(ujinga)ambao mimi kwa mtazamo wangu siamini kama inawezekana katika nngwe hii tunapaswa kufikri hivyo.kuna shule imejengwa afrika ya kusini ambayo imeleta mzozo na hata mimi ninasahangaa kwanini mtoto wa afrika hapaswi kuwa na elimu ila ni wale tu ambao wanaruhusiwa na mlengo huu kuwa wajuzi na sisi kuwa wajinga!!!!!Ndesanjo na bwana egedio na wengine hebu tufikiri kidogo(hivi kuwa na kibali cha kukaa ulaya ,amerika na mabara yote tuyajuayo kinaweza kuwa thamani wa utu wetu?mimi siamini na itakuwa ngumu sana kuamini hivyo.)Nikiendelea na bwana Lufulondama baada ya mwaka huo wa 2000 huko mbinga mkoa wa Ruvuma alifanya kazi hiyo na hatimaye alipata kazi katika mahakama ya wilaya ya Maswa kama Registry officer (afisa masijala wa wilaya)kuanzia 22/10/2002 na kwa sasa baada ya miaka hiyo anasoma katika chuo kinachotambulika cha elimu ya juu(IFM)akiwa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza.Namalizia kwa kusema ELIMU NI MALI;UTAIPATAJEEEEEEEEEEE
karibuni
chuki ikiingia ndani kupitia mlangoni upendo hutoka nje kupitia dirishani,upendo unagharama sana ukilinganisha na chuki,afadhali kununua upendo kuliko kuzawadiwa chuki na migogogro
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Kweli hapo Umenena Elimu ni mali.Mimi elimu ya Bongo hasa ya elimu ya juu bado inatia kizunguzungu sana.Hakuna vitendea kazi,unaaa mwingi,kupiga chabo kwa sana na miyeyusho mingi sana ambayo haiishi kila kukicha vyuoni
Post a Comment