Waziri mkuu wa serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Edward Lowasa ametangazwa na spika wa Bunge Mh Samwel Sitta kuwa amejiuzulu katika kiti hicho cha Uwaziri.
Habari zilizoifikia bongo5 hivi punde zimesema kuwa hatua iliyochukuliwa na Mheshimiwa Lowasa ni dhahiri inatokana na kashfa inayomkabili baada ya kuhusika kuibeba kampuni ya Richmond Development LLC inayodaiwa iko jijini Huston nchini Marekani katika mchakato wa upatikanaji wa zabuni ya umeme wa dharura hapa nchini.
Aidha uthibitisho huo kuhusiana na Mh Lowasa kutia mkono wake katika mchongo huo, ulitolewa na kamati teule ya bunge kwa ajili ya kuchunguza suala hili ikiongozwa na Dr Mwakyembe, ambapo ndani yake ndio ikabainika kuwa mtu mzima alihusika kwa namna moja au nyingine katika kuhakikisha lengo lao linatimia.
Pamoja na Mheshimiwa Lowasa kujiuzulu kama ilivyotangazwa lakini imedaiwa kuwa taarifa bado hazijamfikia mkuu wa nchi Rais Jakaya Kikwete, mwisho Spika amelitaka Bunge tukufu kuendelea kuijadilia ripoti ya Richmond na sio mjadala wa Lowasa na hicho ndio kinachoendelea huko Bungeni kwa hivi sasa.
No comments:
Post a Comment