karibuni
chuki ikiingia ndani kupitia mlangoni upendo hutoka nje kupitia dirishani,upendo unagharama sana ukilinganisha na chuki,afadhali kununua upendo kuliko kuzawadiwa chuki na migogogro
January 14, 2007
Ninaanza kwa kumshukuru sana bwana ndesanjo Macha kwa habari tamu juu ya muziki wa afrika na makala iliyotumwa na bwana Fredy Macha wa stanford bridge kwa makala yake hususani kwa msanii Vitalis Maembe.pia ninashukuru kwa marekebisho yaliyotolewa kuhusiana na jina Halisi la msanii huyu.Labda niwape kwa kifupi historia ya mwanasanaa huyu.Vitalis Maembe mwenyeji wa mkoa wa Rukwa aliyekulia katika jiji la Dar es salaam pale mtoni mtongani ambaye ni mkurufunzi wa chuko cha sanaa Bagamoyo aliyejiunga na chuo hicho mwaka 1998 mwezi wa nane akiwa na wasanii wengine mahiri kama paul Ndunguru, Elidady Msangi,Hussein Masimbi na wengine wengi.vitalis anafahamika kwa umahiri wake wa kuvaa husika katika michezo ya kuigiza pamoja na upendo wake wa sanaa ya mwafrika,Vitalis amekuwa mstari wa mbele kuwatetea watoto yatima na watoto wa mitaani ambao hawana uwezo wa kujikimu katika mahitaji yao ya kawaida,hii imedhihirika katika michoro aliyokuwa akiitengeneza kwani kila wakati alipoamua kutoa mchoro basi mchoro huo ulikuwa ukihusu aidha kupinga utoaji wa Mimba,baa la njaa, maafa ya mafuriko na mambo mengi yanayowalenga watoto.Vitalis alijiingiza zaidi katika sanaa ya muziki hasa mwaka 1999 wakati walipounda kundi lililojulikana kama MANYANI BAND likiongozwa na Paul Ndunguru ambalo lilizua umaarufu mkubwa na kufanya maonyesho kadhaa na bendi kama wana njenje na nyingine nyingi.wasanii waliounda kundi hilo walikuwa ni Paul Ndunguru(msanii mwenye vipaji mbalimbali mdogo wa msanii maarufu philip Ndunguru ambaye ndiye muhasisi wa vikatuni katika gazeti maarufu linalojulikana kama sani),Fredi sagandaNtogwisangu aliyejulikana kama saganda bwai ambaye ndiye muasisi wa miziki yenye ghani ya kiasili.kama mmewahi kusikia wimbo unaoitwa RAPHAELI(nitauinua nikiupata) uliokuwa katika lafudhi ya kichaga(nyumbani kwa akina Ndesanjo)na baada ya hapo ndipo wasanii wengine waliingia na kufuata nyao zake katika nyimbo kama tanga kunani na wagosi wa kaya na mi mmasai na Ebbo Motika anayetokea ngaramtoni katika mji wa kitalii wa Arusha.Vitalis Maembe ambaye alikuwa rais wa chuo cha sanaa Bagamoyo,Elidady msangi na Hussein Masimbi ambaye ni mkufunzi wa chuo cha sanaa.Kundi hilo halikutenga jinsia kwani kulikuwa na akina dada wasanii ambao pia walikuwa ni miongoni mwa waasisi wa kundi hilo kama Pili malundila ambaye sasa ni msanii wa kunndi lijulikanalo kama MIYONZI na HONORATA Ngítu ambao wote ni wahitimu wa chuo cha sanaa chini ya uongozi wa mwana hisimu mashuhuri aliyekuwa mkuu wa chuo hicho Amani Peter Nyambasi.Umahiri wa vitalis Maembe Hukuanzia katika chuo hicho cha sanaa bali ni ni kipaji alichokuwa nacho hata kabla ya kujiunga na chuo hicho kwani tayari alikuwa na kikundi chake cha sanaa pamoja na timu ya mpira wa miguu pale mtoni Mtongani kabla ya kujiunga na chuo hicho ambapo upeo wake wa sanaa uliboreshwa na kutiwa nakshi hadi kufikia katika hatua aliyo nayo sasa.nitaendelea kuwapatia nyeti kuhusiana wa wasanii hawa pindi nitakapopata mpya zihusianazo na maendeleo yao kisanii.ukitaka kujua au kujionea mwenyewe kazi za kisanii za muhasisi wa kundi la manyani na msanii mahiri mwenye vipaji zaidi ya unavyofikiri,tembelea anwani hii http://www.artshost.org/rafiki/rafiki/artists/paul.htm Ninawatakia wakati mwema na afya njema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
Asante kwa kutupa undani kuhusu Vitalis na pia kuhusu Richard Mziray.
unakaribishwa sana bwana Macha Ndesanjo,kumbuka ni wewe uliyenifanya niweze kuyaleta haya kwa jumuia hii,labda ningekushukuru wewe kwa kuniwezesha na pia ninatukumia salamu kutoka ujerumani
bwana egedio ninataka kukuongezea utamu wa hali halisi,nimepokea zawadi ya kachupa kazima ka konyagi kutoka unakojua inakotengenezwa nimekaweka hadi pale ndizi zako za kusukumia pilau zitakapotua ili nako kakusaidie kuteremsha utamu huo.
Post a Comment