karibuni

chuki ikiingia ndani kupitia mlangoni upendo hutoka nje kupitia dirishani,upendo unagharama sana ukilinganisha na chuki,afadhali kununua upendo kuliko kuzawadiwa chuki na migogogro

May 03, 2007

LAWAMA ZA WAKULIMA WA KIAFRIKA ULAYA

Wakulima wa Kenya wailalamikia Ujerumani
Hofu imezidi miongoni mwa wakulima wa Kenya kwamba mabadiliko ya kibiashara kufuatia mkataba mpya kati ya mataifa yanayoendelea na Umoja wa Ulaya, huenda yakawasukuma katika umaskini zaidi.

Mkataba baina ya Umoja wa Ulaya na mataifa yanayoendelea unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mwanzoni mwa mwaka ujao, ni sehemu ya mikataba ya kiuchumi kati ya umoja huo na nchi za Afrika, Caribean na Pacific, ACP. Wajumbe wa mashirika kadhaa ya wakulima nchini Kenya waliandamana nje ya ubalozi wa Ujerumani mjini Nairobi mwishoni mwa juma lililopita wakiitaka serikali ya Ujerumani ichukue hatua kumaliza tabia ya Umoja wa Ulaya kutaka kuwepo mikataba inayozinyanyasa nchi zinazoendelea.

Wakulima na watetezi pia walijadili njia za kuishawishi serikali ya Kenya iwazuie wanasiasa kusaini mkataba huo wa kiuchumi. Wameueleza mkataba huo kuwa usio na haki na usiojali mahitaji ya mataifa maskini. Mazungumzo yanapangwa kufanyika kati ya serikali za mataifa ya Afrika, Caribean na Pacific na Umoja wa Ulaya. Mikataba mipya ya kiuchumi itachukua nafasi ya mkataba wa Cotonou utakaomalizika tarehe 31 mwezi Disemba mwaka huu.

Mkataba wa Cotonou uliosainiwa mwaka wa 2000 nchini Benin ulichukua nafasi ya mikataba mingine ya miaka ya 70 ambayo ilizipa bidhaa kutoka mataifa ya Afrika, Caribean na Pacific, uhuru mdogo wa kuingia soko la Ulaya. kwa mfano asilimia 97 ya bidhaa za Kenya zinazouzwa katika nchini za Umoja wa Ulaya zina haki ya kuingia bila kutozwa ushuru, ikiwa ni pamoja na bidhaa za kilimo cha bustani kama vile maua, ambazo kwa mujibu wa wizara ya biashara na viwanda ya Kenya zimeongeza mapato ya kigeni nchini humo.

Lakini kwa mujibu wa miaktaba mipya ya kiuchumi, hali itabadilika Bidhaa kutoka mataifa ya ACP zitaachwa zishindane na bidhaa za mataifa yenye uwezo mkubwa katika uzalishaji wa bidhaa na huduma. Wakulima wa Kenya pia wameelezea wasiasi wao juu ya hatua ya Umoja wa Ulaya kuendelea kuwapa ruzuzku wakulima wake. ´Tuna wasiwasi kwamba nchi yetu itakaposaini mkataba wa kiuchumi, bidhaa zetu zitakabiliwa na mashindano makali kutoka kwa bidhaa za Ulaya,´ umesema muungano wa wakulima wadogo wadogo, KSSPA, nchini Kenya.

Muungano wa KSSPA unaitaka serikali ikatae kusaini mkataba huo mpaka Wakenya wahakikishiwe kwamba soko lao halitaingizwa bidhaa nyingi na kwamba tatizo la gharama kubwa za uzalishaji bidhaa litashughulikiwa kuwawezesha wakulima kushindana katika masoko ya bidhaa.

Makundi ya kijamii yanawaunga mkono wakulima na yameishauri serikali iwe na uangalifu kuhusu mkataba huo mpya wa kiuchumi. ´Sharti tuhakikishiwe kwamba mkataba mpya wa kiuchumi hautatumaliza. Mapato ya wakulima na wazalishaji bidhaa lazima yalindwe,´ amesema Peter Aoga wa Econews, shirika linalohusika na maswala ya kibiashara mjini Nairobi.

Licha ya hali hii ya wasiwasi miongoni mwa wakulima, serikali ya Kenya imesema itasaini mikataba mipya ya kiuchumi baina ya mataifa ya Afrika, Caribean na Pacific na Umoja wa Ulaya. Katibu mkuu wa wizara ya biashara na viwanda, bwana David Nalo, amesema ni muhimu kufanya kila juhudi kusaini mkataba huo kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Josephat Charo

1 comment:

luihamu said...

Salaam Kutoka kwa Haile Selassi I.
Mimi naitwa Ras Luihamu.

karibu sana,nimefurahi kufahamiana na wewe.

kari ndani ya nyumba ya Haile Selassi I.