karibuni

chuki ikiingia ndani kupitia mlangoni upendo hutoka nje kupitia dirishani,upendo unagharama sana ukilinganisha na chuki,afadhali kununua upendo kuliko kuzawadiwa chuki na migogogro

June 30, 2007

FURAHA

Leo ni siku ya uhuru wa jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo, ninaelekea huko kukutana na waafrika wenye wakati mgumu sana wa kukabiliana na hali halisi ya ukweli wa urangi.nimeahidiwa kupata moja moto na moja baridi hivyo ninafikiri leo jioni nitakuwa tirarira kwa raha ya kukutana na wazalendo wenzagu.wakati huo huo leo pia ni siku ya kusherehekea uhuru wa kameruni na zaidi ya hayo leo pia katika jiji la munik kuna sherehe ya waafrika wanaotoka Afrika ya mashariki.kwa mtaji huo leo ni siku ya mitungi na kama alivyosema J nature ni kwamba HAKUNA KULALA HATA KAMA HUJALA:nawatakia kila la heri.ngoja nikimbie nisije nikapitwa.

2 comments:

luihamu said...

Greetings Kingo,

Nakutakia sikukuu njema lakini kumbuka kuvaa nguo za ushindi.

amani Mzee Kingo.

luihamu said...

Ras,mbona kimya sana?

AMANI RAS.