karibuni

chuki ikiingia ndani kupitia mlangoni upendo hutoka nje kupitia dirishani,upendo unagharama sana ukilinganisha na chuki,afadhali kununua upendo kuliko kuzawadiwa chuki na migogogro

October 12, 2007

MADEREVA WA TRENI WAGOMA UJERUMANI


Kama ilivyokuwa kawaida kwa nchi zinazoendelea kuandaa migomo ya aina mbali mbali,madereva wa Treni hapa jimboni munich wamegoma kufanya shughuli za usafirishaji kwa siku moja kuanzia jana saa sita usiku hadi leo saa sita usiku wakidai ongezeko la asilimia 30 ya mshahara wanoupata kwa madai kwamba mishahara yao ya sasa haikidhi mahitaji yao muhimu.Mgomo huo unahusisha wafanyakazi walioajiriwa na shirika la reli la ujerumani (Deutsche Bahn)hivyo kusababisha huduma za treni mikoani na zile nje ya mikoa kusimama kabisa.wafanyakazi wa shirika la reli katika jimbo la munich hawakuhusika na mgomo huo hivyo usafiri wa mabasi na treni za ardhini kadhalika treni za mitaani(street trains) unaendelea kama kawaida.wafanyakazi wakaao nje ya jiji la munich wamelalamika kwa kuchewa au kutokwenda kabisa kazini kutokama na mgomo huu hasa wale wasio na magari wanaotegemea usafiri wa treni.

2 comments:

luihamu said...

Kilichonivutuia katika picha hiyo ni usafi,naona huko nikusafisana.
Jah live.

kingo said...

huku ni kusafi sana ras, la msingi ni kwamba fungu linalotolewa kwa ajili ya shughuli za usafi linatumiwa vema,huko kwetu si unajua mapanga yanapita halafu kidogo kinachobaki ndo kinatumika kusafisha miji.