Haya wahenga walisema "KIZURI CHAJIUZA NA KIBAYA CHAJITEMBEZA." Uhakika wa msemo utakamilika kwa wawili hawa ambao pingu za maisha zitafungwa kwa kishindo tarehe 14/02/2009 katika kanisa katoliki la Mt. Martha Mikocheni katika jiji la Dar es salaam.Tukianza na mme mtaarajiwa, anakwenda kwa jina la Emmanuel Ngalapa mzaliwa wa mkoa wa Dar es salaam lakini ni mwenyeji wa mkoa wa Morogoro(mji kasoro bahari)wilaya ya Ifakara(huko kuna mpunga kweli kweli).Yeye ni mtangazaji katika kituo cha RADIO MARIA TANZANIA kuanzia mwaka 2005. Mchumba wake ambaye ningependa kumwita mke mtarajiwa, anakwenda kwa jina la Laura John, mwenyeji wa mkoa wa Iringa(kule kwenye baridi sana) lakini amekulia na kupata elimu yake jijini Dar, na kwa sasa ni msomi wa chuo kikuu yalipo makao makuu ya Tanzania Dodoma(Dodoma University).Kingine cha muhimu ni kwamba wapendanao hawa wote wawili ni waimbaji wa kwaya ya kanisa katoliki la Mt.Kizito pale makuburi Dar(kama sijakosea ni mitaa ya tabata hii)na kwaya hiyo ndiyo itakayosindikiza ndoa hii na baadaye kwenye tafrija itakayofanyika katika ukumbi wa Travertine pale magomeni(wengi hupaita migomigo).
La msingi hapa ni kuwapongeza wawili hawa kwa kuonyesha mfano halisi wenye busara wa kufunga ndoa na kuishi kama mke na mume na si mahawara kama ilivyo kwa wengi,ndoa si kitu cha mchezo kwa kuwa ni kutimiza amri ya Mungu na kudhihirisha kukua kiakili na kimwili pia,ahadi ya ndoa inafahamika kwa kuwa natumaini wengi mmeshahudhuria ndoa kadhaa na si rahisi kuifuata kama wapendanao hawajaridhia na kuahidiana wao mwenyewe kwanza kisha mbele ya mashahidi kanisani.wenzangu tulioko huku ughaibuni tunafahamu kuwa ndoa zinafungwa kila siku na talaka zinamiminika kila siku sababu nitawaambia siku nyingine.Natumaini bwana Michuzi utakuwa pale kuwatwanga picha.
Ninawatakia kila la kheri katika maisha yao mapya ambayo si rahisi hata kidogo ingawa yanawezekana.Mengine mtaambiwa na padre pale kanisani.Na wengine waliobaki kufanya hivyo basi tuanze kufikiri kuwa umri hauna reverse geer

4 comments:
Asante sana kwa picha na jina lake Laura ni la mke wa Rais George W. Bush hapa America. Ni jina lenye mategemeo mema. Kwa kutumia Psychology niliyosoma ya kusoma tabia za watu kwa kuwaangalia maumbile yao mke uliyepata ni mke mwema utajionea baadaye. Ile facial impression na appearance mimi nimeridhika navyo. Ila sasa ni vizuri kuongeza maombi maana shetani anawajaribu watu wa Mungu wale ambao ni wake hana haja ya kuwatia kishawishi maana alisha wafuga. All the best
Cornel Shirima
samahani kwa makosa nilimaanisha unatoka Rombo pole sana shirima.karibu ujerumani
Kila la kheri kwa Bibi na Bwana harusi watarajiwa.
Post a Comment